Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi-CCM, Bara, John Mongella akiwa ziarani Mkoani Shinyanga amehani msiba wa aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga,Hamis Mgeja aliyefariki dunia tarehe 03 Novemba, 2025.
Sambamba na hilo, Mongella akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, ametumia nafasi hiyo kutoa salamu za pole, iliyoambatana na Dua ya kumuombea marehemu kutokana na weledi wake ndani ya CCM.


