Dar es Salaam. Wakati mjadala kuhusu operesheni za Rais wa Marekani Donald Trump ukishika kasi katika majukwaa ya dunia, Marekani imezindua mradi wa upanuzi wa kambi yake ya kijeshi ya ukanda wa Afrika Mahsriki iliyo karibu na eneo la mpaka wa Kenya na Somalia.
Mradi huo uliolenga upanuzi wa uwanja wa ndege katika kambi hiyo uliozinduliwa Alhamis 29, 2026 na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Christopher Landau, umetajwa kuwa ni mkakati wa Taifa hilo katika kuimarisha shughuli za kupambana na ugaidi katika eneo la Pembe ya Afrika.
Katika maelezo yake alipozindua mradi huo Alhamisi iliyopita,Naibu Waziri Landau amesema kituo hicho cha ulinzi kinawakilisha ahadi ya wazi ya mkakati wa ulinzi wa pamoja kati ya mataifa hayyo mawili ya Marekani na Kenya. Shirika la Utangazaji la Ujerumani (DW) limeripoti kutoka Kenya.
Licha ya kuwa Marekani imeendelea kuwa na kambi zake za kijeshi katika maenbeo mbalimbali duniani yakiwemo mataifa matano ya Afrika, mradi wa kuiimarisha jeshi la Marekani nchi Kenya umekuja siku chache baada ya kuripotiwa shmabulizi la kigaidi lililohusishwa na kikundi cha Al-shabaab, ambapo watu watatu waliripotiwa kuuawa.
Hata hivyo, licha ya ujumbe wa Marekani kuwa wazi kuwa mkakati huo unalenga kuongeza nguvu za kukabiliana na vikundi vya uasi vya Al-shabaab, baadhi ya wachambuzxi wa masuala ya siasa na uhusiano wa kimaifa wanasema Marekani inaweza kuwa na mpango wa kujihami zaidi na mataifa ya mashariki ya kati kupitia mradi huo.
Kwa muda mrefu, Kambi ya jeshi la anga ya Manda Bay imekuwa eneo la Jeshi la Ulinzi la Kenya katika Kaunti ya Lamu linalotumiwa na vikosi vya Marekani ikiwa kitovu cha kimkakati katika mapambano dhidi ya kundi la itikadi kali la Al-Shabaab lenye mahusiano na Kundi la kigaidi la Al-Qaeda.
Kihistoria, tangu mwaka 2024, Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden alitangaza mipango ya kuifanya Kenya kuwa mshirika mkuu wa kijeshi katika eneo Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, na akaongeza uhusiano wa kijeshi na wa kidiplomasia.
Inrpotiwa kuwa katika uzinduzi huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Christopher Landau, pia ameipongeza Kenya kwa mchango wake kwenye vikosi vya kimataifa katika kuleta utulivu maeneo mbalimbali akiitaja Kenya kama mshirika muhimu katika katika misheni ya kusaidia kupanga vikosi vipya vya kuyaangamiza magenge ya uhalifu katika ukanda huo.
Mchambuzi wa Masuala ya siasa na uhusiano wa Kimataifa, Dk Conrad Masabo, akizungumzia mkakati huo wa Marekani alipozungumza na Mwananchi kwa simu Januari 31, 2026 amesema mkakati wa Marekani unaweza kuwa umelega mikakati ya kiusalama dhidi ya migogoro ya Mashariki ya Kati.
“Marekani inakadiriwa kuwa na vikosi zaidi ya 800 duniani kote, huku kwa Afrika inavyo vikosi vikubwa vitano katika nchi za Djibout, misri, Nigar (alizifunga mwaka jana), Cameroon na hicho cha Kenya, hivyo hii siyo mpya. Lakini, Trump anaahidi kutumia karibu dollar milioni 70 kupanua kikosi chake Kenya, hali inayofanya hoja yake ya Alshaabab ikuwa si kweli kwani angepambana nao hata akiwa Djibout,” amesema.
Mhadhiri huyo wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), amesema hatua hiyo ya Marekani kujiimarisha kijeshi kwa Kikosi cha Kenya haipaswi kufikiriwa kwa hofu na mataifa ya ukanda huu, akiitasja kuwa inaweza kuwa imelenga zaidimataifa ya Mashariki ya Kati.
“Nachokiona kwakuwa kambi yake ya Djibout ipo jirani na kambi ya Wachina, nadhani ni mkakati wa kuongeza operesheni zake akiwa Kenya ambapo atakuwa huru zaidi kukabiliana na mataifa ya Mashariki ya Kati kuliko Djibout ambapo kuna kambi za mataifa mengine makubwa duniani,” ameongeza.
Mwanazuoni huyo pia amehusisha upanuzi huo na kuhamishia nguvu za Marekani hapo kama moja ya mkakati wake kufuatia kufunga kambi zake mbili za Niger, akisema; “unaweza kuwa mpango wake kuimarika kijeshi dhidi ya mataifa ya mashariki ya kati kwani hapo siyo mbali sana, hasa ulinzi wa mfereji wa Kanali ambo ni eneo la kimkakati kwa nchi nyingi duniani,” amesema.