UBUNGO YAREJESHA KAMPENI ‘KAUSAPEU’ KIVINGINE

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam Albert Msando  akizungumza wakati wa zoezi la usafi katika Kata ya Goba jijini Dar es salaam sambamba na uzinduzi wa Kampeni ya Kataa Uchafu Safisha Pendezesha Ubungo (KAUSAPEU)

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam Albert Msando akishiriki zoezi la usafi katika Kata ya Goba jijini Dar es salaam sambamba na uzinduzi wa Kampeni ya Kataa Uchafu Safisha Pendezesha Ubungo (KAUSAPEU) ambalo limefanyika leo tar 31/1/2026

Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafishaji Manispaa ya Ubungo Lawi Bernard akizungumza wakati wa zoezi la usafi katika Kata ya Goba jijini Dar es salaam sambamba na uzinduzi wa Kampeni ya Kataa Uchafu Safisha Pendezesha Ubungo (KAUSAPEU) ambalo limefanyika leo tar 31/1/2026

Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Laurent Mlaki akizungumza wakati wa zoezi la usafi katika Kata ya Goba jijini Dar es salaam sambamba na uzinduzi wa Kampeni ya Kataa Uchafu Safisha Pendezesha Ubungo (KAUSAPEU) ambalo limefanyika leo tar 31/1/2026

Baadhi ya wadau mbalimbali walioshiriki kwenye zoezi la usafi katika Kata ya Goba jijini Dar es salaam sambamba na uzinduzi wa Kampeni ya Kataa Uchafu Safisha Pendezesha Ubungo (KAUSAPEU) ambalo limefanyika leo tar 31/1/2026

…………

NA MUSSA KHALID

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mkoani Dar es salaam Albert Msando amewasisitiza viongozi wa mitaa,Kata na Halmashauri kwa ujumla kuhakikisha wanadumisha na kusimamia suala la usafi linakuwa endelevu ili kuepukana na changamoto za kiafya zinazosababishwa na uchafuzi wa mazingira.

Pia amewataka wananchi kujijengea mazoea ya kufanya usafi mara kwa mara kwenye maeneo yao kwani suala la utunzaji wa mazingira sio hiari bali ni utekelezaji wa shEria.

Mkuu wa Wilaya Msando amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa zoezi la usafi katika Kata ya Goba sambamba na uzinduzi wa Kampeni ya Kataa Uchafu Safisha Pendezesha Ubungo (KAUSAPEU)

Aidha ameagiza kandarasi za ukusanyaji taka zichukuliwe kutoka kwa wakandarasi wasiofanya kazi na kupewa vikundi vya vijana na wanawake kupitia mikopo ya asilimia 10 ili kuboresha usafi na kuinua uchumi kwa jamii.

Awali akizungumza Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Laurent Mlaki amewasisitiza wananchi kuendelea kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yao ambapo itakwenda sambamba na utoaji wa tuzo katika kata ambayo itafanya vizuri katika zoezi hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafishaji Manispaa ya Ubungo Lawi Bernard amesema kuwa lengo lao ni kuendelea kuhamasisha jamii kufanya usafi kwenye maeneo yao ili wawe salama kwa afya zao.

‘Kampeni hii kama ilivyotambulishwa na Mstahiki Meya inakwenda kushindanisha mitaa ambapo kwa kila baada ya tathmini mtaa uliongoza unapatiwa zawadi ya fedha ili kutoa motisha sababu wamekuwa machampioni lakini ukiwa wa mwisho unapewa bendera ya balozi wa uchafu ambayo itawekwa kwenye ofisi ya mtaa haishushwi mpaka tathmini ifanyike’amesema Lawi

Aidha ametoa rai kwa wananchi kutii sharia bila shuruti kwani kuliko kupigwa faini kwa kosa la kufanya uchafuzi wa mazingira ni bora wakaongeza jitihada katika kufanya usafi ili kuyatunza maeneo yao yanayowazunguka.

Pia Lawi ameeleza kuwa wataendelea kutoa elimu ya mazingira kwa jamii ikiwemo kusimamia sharia ndogo ndogo za usafi ili kuhakikisha Ubungo inakuwa Manispaa ya Mfano katika suala la usafi.

Ikumbukwe kuwa Kampeni ya KAUSAPEU imerejea kwa mara nyingine ikiwa ni baada ya kufanyika na kuonyesha mafanikio makubwa katika mitaa na kata mbaimbali kwa jamii kuelimishwa na kushiriki katika zoezi la ufanyaji wa usafi kwenye maeneo yao.