Lugola ahoji uhuru wa Polisi na DPP, awashukia ‘machawa’
Dodoma. Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amesema ili kumaliza mafisadi na wabadhirifu nchini na kuipata ‘Tanzania mpya’, ni lazima vyombo vya dola, kwa maana ya Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), viwe huru. Mbali na hayo, amesema watu aliowaita ‘machawa’ ndiyo wameifikisha nchi hapa, akitaka wabunge wawe huru wasibanwe,…