Dili zikitiki Tanzania Prisons kazi mnayo!
VIONGOZI wa timu ya Tanzania Prisons wanaendelea na vikao vya tathmini mkoani Dodoma, ili kupata picha ya kipi wakifanye katika usajili wa dirisha dogo litakalofungwa Januari 30, lakini kama michongo yao itatiki wapinzani waliopo katika Ligi Kuu Bara itabidi wajipange mapema. Prisons imecheza mechi saba imeshinda mbili, imetoka sare moja na imefungwa nne, imekusanya pointi…