TANESCO YAWEKA WAZI TARATIBU ZA UPIMAJI NA MAUNGANISHO YA UMEME RUVUMA.
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ruvuma, Allen Njiro, amesema kuwa wananchi hawatakiwi kulipa fedha zozote kwa maafisa wanaofanya upimaji wa umbali wa kufikisha huduma ya umeme, kwani kazi hiyo ni sehemu ya majukumu ya watumishi wanaolipwa na serikali. Njiro ameyasema hayo leo Januari 29, 2026, wakati…