Biashara chuma chakavu inavyoathiri miundombinu ya umeme
Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Lazaro Twange, amesema licha ya Serikali kufanya uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya umeme, changamoto kubwa inayokwamisha juhudi hizo ni biashara ya chuma chakavu, ambayo imekuwa tatizo katika kulinda miundombinu hiyo. Kauli hiyo alitoa leo Januari 6, 2026 mbele ya Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi,…