Dereva aliyefungwa Sudan arejea nchini, asimulia

Dar es Salaam. Nderemo na machozi ya furaha vilitawala jijini Dodoma, wakati wa mapokezi ya Juma Maganga, dereva Mtanzania aliyekuwa amefungwa nchini Sudan Kusini. Maganga alikuwa kizuizini tangu Februari 14, 2025 baada ya gari alilokuwa anaendesha kumgonga na kusababisha kifo cha mwanajeshi. Alitakiwa kulipa faini ya ng’ombe 51 (sawa na Sh36 milioni) kwa mujibu wa…

Read More

Mtego wa Yanga upo hapa, Pedro atia neno

BINGWA mara mbili wa Kombe la Mapinduzi na bingwa wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara, Yanga SC, leo Jumapili inatupa karata yake ya kwanza dhidi ya KVZ. Hiyo itakuwa saa 10:15 jioni katika mechi ya kundi C kwenye michuano ya Mapinduzi Cup 2026 inayochezwa Uwanja wa New Amaan Complex uliopo Unguja. Yanga ikiwa inaanza kutupa…

Read More

Straika aipa mechi tano Transit Camp

STAA wa Transit Camp, Adam Uledi amesema licha ya kuongoza katika Ligi ya Championship kwa idadi ya mabao, lakini matokeo waliyonayo hayaendani na mahitaji akizitaja mechi tano tu zitakawapa mwanga maafande hao kupanda Ligi Kuu Bara. Nyota huyo aliyewahi kung’ara akiwa Ken Gold kwa misimu miwili akiwa kinara wa mabao kikosini, ameendelea kuonyesha makali mbele…

Read More

Patashika wanafunzi wakirejea shuleni | Mwananchi

Dar/Moshi. Maandalizi ya wanafunzi kurejea shuleni yakipamba moto, imeelezwa kuwapo shida ya kupata vitabu vya mtalaa mpya. Kwa mujibu wa ratiba, shule za msingi na sekondari nchini zitafunguliwa Januari 13, 2026. Ufuatiliaji uliofanywa na Mwananchi Januari 2, 2026 katika baadhi ya maeneo ya Kariakoo, Karume na Mbezi Mwisho unaonyesha uwepo wa idadi kubwa ya watu…

Read More

Alliance yatimua kocha, yamrejesha Mirambo

TIMU ya Alliance FC ya jijini Mwanza imemrejesha kocha wake wa zamani, Mirambo Camil kuongoza benchi la ufundi baada ya mwenendo usioridhisha katika First League. Kocha huyo ambaye amekabidhiwa timu tangu Desemba 30, 2025 akiwa na leseni ya Diploma A ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), anachukua mikoba ya Chikaka Julius ambaye ametupiwa virago kutokana…

Read More

Serikali yatenga Sh125 bilioni kujenga mabwawa

Dar es Salaam. Serikali imetenga Sh125 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa saba katika mikoa ya Morogoro na Dodoma baada ya upembuzi yakinifu kukamilika. Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo amesema hayo alipopewa nafasi na Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba kuwasalimia wakazi wa Gulwe, Mpwapwa mkoani Dodoma. Dk Mwigulu jana Januari 2, 2026 alifanya ukaguzi wa…

Read More

LUSWETULA: SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA UFANYAJI BIASHARA NCHINI

Na Benny Mwaipaja, Mpanda Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), ameihakikishia jumuiya ya wafanya biashara na wajasiriamali nchini kwamba Serikali itaendelea kuwawekea mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara ili kukuza biashara zao. Mhe. Luswetula ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na jumuiya ya wafanyabiashara mjini Mpanda mkoani Katavi ambapo amesisitiza kuwa hatua hiyo…

Read More