Massanza: Guede ananikumbusha Sowah | Mwanaspoti
OFISA Habari wa Singida Black Stars, Hussein Massanza, amesema moto alioanza nao mshambuliaji wa timu hiyo, Joseph Guede, unamkumbusha alivyokuwa Jonathan Sowah. Guede ambaye amerejea Singida Black Stars baada ya awali kuitumikia kwa takribani miezi mitano msimu wa 2024-2025, ameanza vizuri kwa kufunga mabao mawili katika michuano ya Kombe la Mapinduzi 2026 inayoendelea kisiwani Unguja…