Ufunguzi wa Ofisi ya CRDB Bank Dubai sasa umeiva, Nsekela Aridhishwa na Utayari wake Katika Kukuza Biashara na Uwekezaji
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, ametembelea Ofisi ya Uwakilishi ya Benki ya CRDB iliyopo Dubai, Falme za Kiarabu, ikiwa ni hatua muhimu kuelekea uzinduzi rasmi wa ofisi hiyo unaotarajiwa kufanyika mapema Januari 2026. Katika ziara hiyo, Nsekela alipokea taarifa ya kina kuhusu utekelezaji wa shughuli za ofisi tangu ilipoanza kazi rasmi Oktoba…