Serikali yahimiza uwekezaji wa ndani, Tiseza ikizindua dawati Mara
Musoma. Serikali imedhamiria kuongeza idadi ya wawekezaji wa ndani kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji baada ya kubaini kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazowakwaza Watanzania wengi kushiriki kikamilifu katika uwekezaji. Hatua hiyo imeonekana kupitia Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi (Tiseza), ambayo imezindua dawati maalumu la huduma mkoani Mara, likilenga kusogeza huduma karibu na wananchi,…