TCAA YAIMARISHA USALAMA WA ANGA KWA MIFUMO YA KISASA
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema imejizatiti kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani, ikiwemo matumizi ya Akili Mnemba (AI), ili kuendelea kuimarisha usalama na ufanisi wa usimamizi wa anga nchini. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi, wakati akifungua Mkutano wa 45 wa Mwaka…