Mikopo ya simu inavyogeuka mkombozi kipindi cha ukata
“Ukisikia ‘Njaanuari’ tarehe kama hizi ndiyo imeshika kasi. Baada ya matumizi makubwa ya sikukuu na likizo za mwisho wa mwaka, unakutana na ada za watoto, kodi ya nyumba, na mahitaji mengine ya lazima. Hapo ndipo unapoanza kutafuta mkopo wa kukuvusha kipindi hiki,” anasema Ismail Hamis, mkazi wa Dar es Salaam. Hamis anasema tofauti na miaka…