Kihongosi: Hatutafumbia macho miradi itakayotekelezwa chini ya kiwango
Iramba. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza hakitanyamaza wala kufumbia macho miradi inayotekelezwa chini ya kiwango, badala yake lazima kipaze sauti. Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Januari 21, 2026 na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi alipokagua ujenzi wa barabara ya Kitukutu – Gumanga – Mkalama – Chemchem – Nyahaa, yenye urefu…