UCHAMBUZI WA MJEMA: Bila Bunge na Mahakama huru, utawala wa sheria ni ndoto

Wiki iliyopita, Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju alitaja mambo manane akitaka yawezeshwe ili kuifanya Mahakama kuwa huru isiyoingiliwa kwenye utoaji haki, na mimi namuongezea kuwa tunahitaji pia Bunge huru litakaoisimamia Serikali. Bila vyombo hivyo kuwa huru, visivyofanya uamuzi kwa shinikizo, maelekezo au maslahi ya kisiasa, kilio cha utawala wa sheria ambacho kinasikika hivi sasa…

Read More

Trump akwaa kisiki Ulaya | Mwananchi

Dar es Salaam. Mpango wa Rais wa Marekani, Donald Trump kuweka vikwazo vya kodi kwa Mataifa ya Ulaya umechukua sura mpya baada ya Umoja wa Ulaya (EU) kuchukua hatua za kulipiza kisasi. Hatua za Trump zilizotangazwa Januari 2026, zinahusu ushuru wa ziada kwa bidhaa za viwandani kutoka Ulaya. Akizungumza nchini Marekani, Rais Donald Trump alisema…

Read More

NIKWAMBIE MAMA: Gharama ya uzembe ni maanguko

Wahenga walisema “Utavuna ulichopanda”. Kama ulipanda mahindi haiwezekani kuvuna mtama hata kama zote ni nafaka. Usemi huu una maana kubwa zaidi na kufanana na “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo”. Malezi ya mtoto yanafananishwa na mbegu iliyopandwa na kuhudumiwa ikiwa ardhini. Ikiwa mbegu ni bora na imepandwa kwenye ardhi yenye rutuba, ni lazima itatoa mazao yanayotarajiwa. Siku…

Read More

Miradi hii iendelezwe isife ‘kifo cha mende’

Wakati wa maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar, miradi mingi ya maendeleo imezinduliwa au kuanza kutekelezwa. Hatua hizi ni ishara chanya ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi. Hata hivyo, kilicho muhimu zaidi ya uzinduzi wa miradi hiyo ni usimamizi wake, pamoja na kuhakikisha inalingana na kiwango cha fedha kinachotumika. Utekelezaji wa…

Read More

Jeshi la Marekani laikamata meli ya Venezuela

Venezuela. Kamandi ya Kusini ya Jeshi la Marekani (Southcom) imeikamata meli ya mafuta inayomilikiwa na Venezuela kwenye Bahari ya Caribbean, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi hilo jana Jumanne Januari 20, 2026. Vikosi hivyo vimesema meli hiyo ya Sagitta, ilikuwa imekiuka marufuku iliyowekwa na Rais Donald Trump. Ukamataji huo unakuja ikiwa ni karibu siku…

Read More

Mdogo wake Niyonzima aiwahi Azam FC

AZAM baada ya jana kumaliza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Fountain Gate, akili yao sasa ipo nchini Kenya ikiwa na kibarua cha kuikabili Nairobi United ambayo imeongeza mashine nne akiwemo ndugu yake Haruna Niyonzima. Azam iliyopo kundi B katika Kombe la Shirikisho Afrika, Januari 25, 2026 itakuwa kwenye Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi…

Read More

KONA YA MALOTO: Siasa ni mihadarati, hupofusha, huumiza na kuua taifa

Msomi wa uandishi wa kibunifu (creative writing), Veronica Roth wa Chuo Kikuu cha Northwester, Marekani, aliandika kwa kuhoji; Tunachangia adui, lakini hiyo inafanya sisi tuwe marafiki? Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Condoleezza Rice, alisema: “Tunahitaji adui mmoja ili atuunganishe.” Mwandishi James Fahy alipata kuandika: “Hakuna kinachoweza kuwaunganisha binadamu kama adui mmoja.” Kilichokuwa…

Read More

Mkongomani kumrithi Chama Singida Black Stars

MUDA mchache baada ya Singida Black Stars kukubali kumwachia Clatous Chama atimkie Simba, uongozi wa klabu hiyo upo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kiungo Mkongomani, Linda Mtange kutoka Aigles Du Congo. Chama aliitumikia Singida Black Stars kwa miezi sita akitua mwanzoni mwa msimu huu akitokea Yanga na alihudumu kwa msimu mmoja akitokea Simba….

Read More

Edwin Mtei; Jina dhahabu Tanzania kisiasa, kifedha

Mchunga mifugo aliyesoma kwa dhamira hadi kuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BOT). Mwanasiasa aliyeanzisha chama kilichopanda hadi kuwa chama kikuu cha upinzani. Mkulima wa kahawa mwenye mafanikio. Mstaafu wa utumishi wa umma aliyeishi maisha yake ndani ya misingi. Edwin Isaac Mbiliewi Mtei. Gavana mwasisi wa BOT. Mwenyekiti mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo…

Read More