Shabiki Ampiga Ngumi Mangungu – Video



Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu jioni ya leo ameingia kwenye ‘kashkash’ baada ya shabiki wa Simba kutaka kumshushia kichapo.

 

Sekeseke hilo limetokea nje ya Dimba la Benjamin Mkapa baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Simba na Esperance de Tunis, Simba ikilazimishwa sare ya 2-2.

 

Askari na maafisa usalama waliokuwepo eneo hilo, walikuwa na kazi ya ziada ya kumnusuru Mangungu dhidi ya shabiki huyo ambapo baadaye hali ilitulia na Mangungu kusindikizwa na askari na maafisa hao.