WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amefanya mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Bi. Beth Bechdol jijini Dar es salaam leo tarehe 3 Februari, 2026.
Pamoja na mambo mengine, Viongozi hao wameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na FAO ili kukuza na kuimarisha sekta ya Kilimo nchini.

