Shule ya Sekondari ya Royal Family iliyopo Manispaa ya Geita imeandika historia mpya katika matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne 2025 yaliyotangazwa rasmi leo Januari 31,2026 na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).
Shule hiyo imefanya vizuri kwa kupata wanafunzi 33 wa Daraja la Kwanza na wanafunzi 3 pekee wa Daraja la Pili huku ikivuna rekodi adimu ya kutokuwa na mwanafunzi yeyote wa Daraja la Tatu,Nne wala Sifuri.
Matokeo hayo yameitambulisha Royal Family Sekondari kama miongoni mwa shule bora zaidi katika Manispaa ya Geita na Tanzania kwa ujumla yakidhihirisha ubora wa taaluma, nidhamu na uwekezaji mkubwa katika elimu.
Miongoni mwa wanafunzi waliopata daraja la kwanza na daraja la pili ni wale waliochujwa kwenye shule zingine kwa kigezo cha kutofanya vizuri na wakapokelewa shule ya sekondari ya Royal Family.
Walimu na wanafunzi wameelezwa kufanya kazi kwa bidii,mshikamano na malengo ya pamoja yaliyowezesha ushindi huo mkubwa usio na doa.
Akizungumza kwa furaha Mkurugenzi wa shule hiyo Mhandisi Lazaro Philipo alisema matokeo hayo ni matunda ya mipango thabiti ya kielimu na ushirikiano wa karibu kati ya walimu,wanafunzi na wazazi.
Aliongeza kuwa mafanikio hayo yanatoa motisha ya kuongeza juhudi zaidi ili shule iendelee kuwa kinara wa ufaulu bora na kuandaa wanafunzi wenye maarifa,maadili na ushindani wa kimataifa.

.jpeg)
.jpeg)
