Tume yakutana na Mganga Mkuu wa Mkoa

TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imekutana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Thomas Rutachunzibwa.

Rutachunzibwa katika mkutano huo wa Tume uliofanyika  katika Ukumbi uliopo katika Jengo la Takwimu lililopo mkoani hapa aliongozana na wataalamu wa afya kutoka ndani yam koa huo.

Miongoni mwa yaliyojadiliwa katika mkutano huyo ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo.

Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali wakiwemo waathirika wa Matukio hayo ambapo kwa Dodoma tume inaendesha shughuli zake katika Ukumbi wa Takwimu, kwa Mkoa wa Iringa Tume ipo Ukumbi wa Siasa ni Kilimo na kwa Shinyanga Tume ipo katika Ukumbi wa Manisapaa ya Kahama.