KATORO YAPOKEA GARI LA ZIMAMOTO

Serikali mkoani Geita imeikabidhi gari la zimamoto mamlaka ya mji mdogo wa Katoro gari ambapo linatarajiwa kuwa Msaada mkubwa kwa wananchi wa mji huo.

Mkuu wa mkoa wa Geita Martin Shigella amezindua gari hilo ambalo lina uwezo wa kubeba jumla ya Lita 5000 za maji ya kuzimia moto pamoja na form compound Lita 500.

Akizungumza na wananchi katika mji huo Shigela amewataka wananchi wa Katoro kulitumia na kulitunza vizuri gari hilo ambalo limekuja kuwa Msaada mkubwa ambapo hapo awali ilibidi kusafiri umbali mrefu kupata Msaada wa zimamoto.

Aidha Shigela ametoa maelekezo kwa mamlaka ya maji kuanzisha vituo vya maji sehemu mbalimbali katika mji huo ili gari hilo lisisafiri umbali mrefu kufata maji kwa ajili ya kuzimia moto.

“Mamlaka ya maji GEUWASA tuhakikishe tunaweka miondombinu ya maji Kila mahali ili vituo vya maji vipatikane Kila sehemu kwa ajili ya kuondoa usumbufu wa kujaza maji kwenye gari hili” alisema Shigela.

Kwa kipindi Cha mwaka 2025 mpaka 2026 mwanzoni jumla ya nyumba 10 na maduka 4 yalipata ajali ya moto ambapo gari ya kuzima moto huo ilikuwa ilikea Geita manispaa.

Jeshi la zimamoto mkoa wa Geita kimetoa wito kwa wananchi kutumia  namba ya dharula ya zimamoto kama ilivyoelekezwa na si kwa mambo binafsi.

Kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na  uoakoaji mkoa wa Geita ASF Kenneth Mwakasitu amesema kupitia namba 114 mwananchi atapata huduma ya zimamoto kwa masaa 24.

“Wananchi tujue matumizi sahihi ya namba hii ya dharula,hatutegemei matumizi mengine ya mzaha au michezo kwasbabu hii namba yetu ni kwa ajili ya kuzima moto na kufanya maokozi” alisema Mwakasitu

Nae mbunge wa Jimbo la Katoro Eng. Kija Ntemi amesema kuwa gari hili linaenda kuwapa ahueni wafanyabiashara katika mji huo ambao wamekuwa wakiishi kwa wasiwasi kutokana na ukosefu wa gari la zima moto katika maeneo ya karibu.