Kesi ya uhaini No. 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu imeendelea leo, Jumatatu Februari 09.2026 kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam
Kesi hiyo inayosikilizwa mbele ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru leo imekuja kwaajili ya upande wa Jamhuri kujibu hoja za mapingamizi yaliyowekwa na mshtakiwa Novemba 12.2025, kesi hiyo ilipotajwa mara ya mwisho Mahakamani hapo
Msingi wa mapingamizi hayo unatokana na shahidi wa siri wa Jamhuri (PW11) na kizimba cha siri cha kuongelea shahidi kilichopo kwenye chumba cha Mahakama
Baada ya Mahakama kusikiliza hoja za pande zote mbili, kesi hiyo ikaahirishwa hadi Jumatano ya Februari 11.2026 itakapotajwa tena, kwaajili ya kutolewa uamuzi wa mapingamizi hayo, na kuendele na ratiba nyingine.
Related
