RUWASA GEITA DC YAFANYA MKUTANO WA NUSU MWAKA NA CBWSO

Jumla ya shilingi milioni 40 hukusanywa Kila mwezi kutoka kwa jumuiya za watoa huduma za maji ngazi ya jamii (CBWSO) katika wilaya ya Geita.

Hayo yamesemwa na meneja wa Wakala wa Maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA wilaya ya Geita  Injinia Sande Batakanwa katika mkutano wa nusu mwaka wa jumuiya za watoa huduma za maji ngazi ya jamii Yani CBWSO katika wilaya hiyo.

Batakanwa alisema kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwa jumuiya hizo katika wilaya hiyo ambapo Sasa wananchi wanapata huduma Bora za maji ambazo zimefuikisha asilimia 60 ya upatikanaji wake katika wilaya ya Geita.

Lusekelo Mwaikenda afisa mtendaji kata ya Nyarugusu amekiri uwepo wa manufaa makubwa kupitia CBWSO hizi ambapo Sasa wananchi wanapata huduma za maji kwa wakati. 

Aidha aliongeza kuwa kufuatia kuwepo kwa mradi wa RUWASA katika kata ya Nyarugusu wananchi wameepukana na adha ya maji katika eneo Hilo ambapo hapo awali walitumi maji ya kwenye mabwawa ambayo si safi na salama.

Nae diwani wa kata ya Kaseme Andrew Kalamula alisema kuwa viongozi katika kata ya Kaseme wamekuwa wakihamasisha utunzajibwa mazingira ili kulinda na kuvitunza vyanzo vya maji na katika kata hiyo.