FCC iendeleni kusimamia ushindani katika soko katika kumlinda mlaji-Naibu Waziri Londo

Kaimu Mkurugenzi Mkuu FCC aweka mikakati ya utoaji huduma zinazoenda na viwango boraWaziri wa Viwanda na Biashara Dennis Londo amesema Tume ya Ushindani (FCC) iendelee na majukumu  ya kusimamia ushindani katika kujenga imani ya walaji kwani sehemu ya huduma ndio wananchi wanapokutana na serikali

Londo aliyasema hayo wakati alipotembelea Tume ya Ushindani Jijini Dar es Salaam,amesema kuwa ushindani katika soko unajenga imani ya walaji kupata huduma zilizo bora na kufanya kuchangia uchumi wa nchi.

Amesema imani ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuona Taasisi ya  FCC inaendelea kulinda ushindani nchini kwa taratibu na sheria zilizowekwa katika kuhakikisha walaji wanakuwa wa kwanza kutoa taarifa sahihi za huduma wanazozipata.

Aidha amesema kuwa katika kuhakikisha  wanalinda soko za bidhaa za ndani kwani Tanzania inafikiwa na mataifa mbalimbali hivyo bidhaa hizo zikitoka zikawa chini ya viwango kunafanya nchi kuathirika na kushindwa kupata fedha za kigeni.

Hata hivyo amesema kuwa wafanyakazi FCC kuendelea kutoa huduma bora ambazo zitachochea uwekezaji wa viwanda vitavyofanya kuendelea kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania.

Amesema matamanio ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuona tija inaendelea kuongezeka katika malengo ya kukua kiuchumi na Dira ya Taifa 2050.

“Nina imani na FCC na Wizara tutaendelea kushirikiana katika kuwafikisha watanzania kwenye kupata huduma bora katika ushindani wa soko wenye uwazi bidhaa za ndani na nje ya nchi”.amesema Londo 

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) Khadija Ngasongwa amesema FCC imejipanga vyema kuendelea kushirikiana na  katika kutekeleza majukumu kwa mujibu wa sheria ili kuendelea kutoa huduma zenye tija kwa mlaji na Taifa kwa ujumla hususan katika masuala ya Ushindani, Udhibiti wa Bidhaa Bandia na Kumlinda Mlaji kwa lengo la kukuza ustawi wa uchumi jumuishi.

Khadija anesema  katika kutekeleza majukumu yetu kwa mujibu wa mamlaka tuliyopewa kisheria, Tume ya Ushindani (FCC) hufanya kazi kwa karibu na Wizara ya Viwanda na Biashara, Idara, Taasisi za Serikali, Wadau wa Maendeleo na Sekta Binafsi kwa kuzingatia dira na miongozo mbalimbali ya kisera, kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha inatekeleza jukumu lake kama chombo cha usimamizi wa utendaji wa ufanisi wa uchumi wa soko kwa kulinda na kushajiisha uzingatiwaji wa misingi ya ushindani wa haki, kumlinda mlaji na kudhibiti bidhaa bandia katika soko la Tanzania Bara. 

Majukumu haya kwa pamoja yanalenga kulifanya soko kuwa shindani, salama na walaji wanajenga uaminifu katika bidhaa zinazoletwa sokoni na hivyo mazingira ya biashara kuchangia ukuaji endelevu na jumuifu katika uchumi na ustawi wa mtu mmoja mmoja.

Amesema FCC ina jukumu la kusimamia Ushindani katika Soko la Tanzania Bara kwa kuhakikisha kuwa inadhibiti makubaliano yanayofifisha Ushindani, matumizi mabaya ya nguvu ya soko na miungano ya kampuni inayolenga kuimarisha hodhi ya soko. Tume imepewa mamlaka ya kisheria ya kufanya uchunguzi endelevu (Inquisitorial Procedure) katika kushughulikia ukiukwaji wa Sheria ya Ushindani ambapo huweza kutoa maamuzi dhidi ya ukiukwaji huo, ikihusisha pia masuala ya kumlinda mlaji.

Aidha, FCC imepata mafanikio makubwa baada ya Marekebisho ya Sheria ya Ushindani  ambapo sasa Sheria hiyo inaweza kufanya maamuzi dhidi ya ukiukwaji wa mashauri yanayohusiana na masuala ya kumlinda mlaji badala ya masuala hayo kufanywa na mahakama pekee.

Aidha amesema  majukumu mengine wanayotekeleza ni pamoja na kuchunguza na kuchukua hatua kwa wafanyabiashara wanaobainika kujihusisha na uingizaji nchini, uuzaji, uzalishaji, usafirishaji na uhifadhi wa bidhaa bandia.

 Amesema FCC inatoa elimu au uraghibishi wa Ushindani  kushajiisha utekelezaji wa Sheria ya Ushindani kwa njia ya mashauriano na maelekezo kwa Taasisi za Umma bila kutumia taratibu za kisheria zenye adhabu mbalimbali. 

Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu amesema FCC inajukumu la kumlinda mlaji dhidi ya mbinu na mienendo kandamizi na hadaifu katika soko, na hivyo kutoa elimu kuhusu haki na wajibu wa mlaji kupitia vyombo vya habari, tovuti na mitandao yake ya kijamii, kutathmini na kusajili mikataba ya walaji inayoandaliwa na upande mmoja na hushughulikia malalamiko ya walaji wa bidhaa na huduma katika soko.

 Amesema  FCC imewezesha na kuimarisha uwekezaji baada ya kuongeza kizingiti cha ulazima wa kuiarifu FCC kuhusu kusudio la kuunganisha shughuli za kibiashara kutoka Shilingi milioni 800 hadi bilioni 3.5 ambapo kampuni za wajasiriamali wadogo na wa kati ambazo thamani ya jumla ya rasilimali zao haifiki kizingiti hicho cha Shilingi bilioni 3.5, zinaweza kuunganisha shughuli zao za kibiashara bila ulazima wa kuomba kibali kutoka FCC. 

Kwa hatua hiyo FCC tumewezesha ukuaji wa biashara ndogo na za kati ambazo zimeweza kuunganisha shughuli zao na kukuza kiwango cha mitaji ya SMEs na kuziwezesha kukopesheka na utafutaji wa teknolojia zaidi, ili kuweza kushiriki zaidi katika uwekezaji na biashara nchini.

 Katika hatua hiyo FCC ya Miungano ya kampuni  imekuwa ikileta faida kubwa katika uchumi wa soko ikiwa ni pamoja na kukuza mitaji ya kampuni husika, kuingia sokoni kwa wawekezaji wapya, kupatikana kwa teknolojia bora za uzalishaji, kuongezeka kwa uzalishaji na tija, kuwezesha upatikanaji wa uchaguzi wa bidhaa na huduma na hivyo kuwezesha bidhaa kupatikana kwa bei za ushindani na kuongeza mapato ya Serikali kwa njia ya kodi.

 Khadija amesema FCC imesogeza huduma karibu kwa kufungua Ofisi za Kanda katika Kanda ya Ziwa (Mwanza), Kanda ya Kaskazini (Arusha) na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya) pamoja na Ofisi ya Tanga.  Baada ya kufungua Ofisi hizo, FCC sasa tuna jumla ya Ofisi sita ikiwa ni pamoja na Dar es Salaam na Dodoma. Ofisi hizi zinawezesha usimamizi madhubuti wa Sheria ya Ushindani pamoja na Sheria ya Alama za Bidhaa kwa ufanisi zaidi.

Khadija amesema FCC imepata Cheti cha Ithibati ya utoaji wa huduma zenye viwango kimataifa, “ISO CERTIFIED 9001:2015” na usimamizi mzuri wa misingi ya Ushindani, kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara na uwekezaji ni jambo tunaloliangalia kwa karibu sana na kuliimarisha na kuwapa wawekezaji imani ya kuwekeza nchini kutokana na FCC kuaminika na kuwa miongoni mwa vyombo vya kusimamia uchumi wa soko, kwa kuhakikisha urahisi wa wawekezaji kuingia na kutoka sokoni bila vikwazo, na kwa kuhakikisha sheria, taratibu na kanuni za ushindani, kumlinda mlaji na kudhibiti bidhaa bandia zinasimamiwa vyema katika soko.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Dennis Londo akizungumza na wafanyakazi wa FCC wakati alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kujua majukumu ,jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa FCC Dkt.Aggrey Mlimuka akizungumza kuhusiana na majukumu yao kuishauri Taasisi yao katika utoaji huduma ,jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu FCC Khadija Ngasongwa akitoa maelezo kuhusisiana na Majukumu ya Taasisi hiyo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara  Dennis Londo wakati alipotembelea Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Dennis Londo akiwa katika picha ya pamoja na makundi ya muundo wa FCC ,jijini Dar es Salaam.