KCB YAUNGA MKONO USAFI SOKO LA DARAJANI ZANZIBAR

Zanzibar 

TAASISI za kifedha na makampuni mbali mbali zimetakiwa kujitowa na kusaidia shughuli za kijamii sambamba na kutenga kiasi cha faida wanazopata kusaidia jamii zinazowazunguuka katika biashara zao.

Usafi ni jukumu la kila mtu hapa Benki ya biashara ya KCB imeamuwa kuunga mkono jitihada za serikali ya Zanzibar katika kudumisha usafi na mazingira wakitambuwa usafi ni Afya.

Mkuu wa Soko la darajani manispaa ya mjini Zanzibar Mariam Juma Mzee amesema hatua hiyo imewapa faraja na kuzitaka taasisi nyengine kuunga mkono usafi katika masoko ili kuendeleza Afya Bora kwa watumiaji sokoni Hapo.

Mariam Juma Mzee – Mkuu wa Soko Darajani Zanzibar .Baadhi ya wafanya Biashara katika soko hilo wameelezea umuhimu wa shughuli za usafi.

KCB wameamuwa kufanya usafi katika maeneo mbali mbali ya soko hilo ili kutowa hamasa kwa wananchi na wafanya biashara kuendeleza usafi.