Mkuu wa mkoa wa Geita ametangaza rasmi kutokuwa na mwekezaji katika eneo la uwanja wa mpira wa CCM, eneo ambalo lilibua taharuki baina ya serikali ya Kijiji na chama Cha mapinduzi.
Ikumbukwe kuwa mnamo January 24 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Mhe Riziki Shemdoe aliuagiza uongozi wa wilaya ya Geita Chini ya mkuu wa mkoa wa Geita kuhakikisha ndani ya siku 14 unawasilisha taarifa ya kina kuhusu mgogoro unaomhusisha mwekezaji aliyedaiwa kubomoa maeneo ya serikali na kuanzisha miradi bila utaratibu.
Akiongea na wananchi katika mamlaka ya mji mdogo wa Katoro mkuu wa mkoa wa Geita Martin Shigela amesema kuwa mwekezaji ambaye alitajwa na kuwekeza katika eneo la chama Cha mapinduzi hakuwa na Mikataba ya kuwekeza katika eneo Hilo.
Shigela amewataka wananchi kuwa watulivu na kusubiri majibu ya vikao vya ndani baina ya chama na serikali ambapo ameongeza kuwa eneo Hilo halipaswi kubadilishwa matumizi ambapo hapo awali eneo hilo lilitumika kama eneo la Michezo
Januari 23,2026 kamati ya FEDHA na uchumi ya halmashauri ya wilaya ya Geita ilifika katika eneo Hilo na kubaini kwamba mwekezaji tajwa alikuwa akiendelea na shughuli za kuanzisha mradi wake bila ya kuwa na vibali ,hali iliyoibua taharuki Kati ya mwekezaji huyo na wajumbe wa kamati hiyo iliyoongozwa na mwenye kiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita Jumanne Misungwi.
Nae mbunge wa Jimbo la Katoro Mhandisi Kija Limbu Ntemi ameushukuru uongozi wa mkoa kwa kusimamia swala hilo ambalo lilianza kuleta taharuki kwa wananchi waishio maeneo hayo