Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera , Bunge ,Uratibu na Wenye Ulemavu Ummy Nderiananga amesema Tanzania inaungana na nychi nyingine duniani katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Breli na maadhimisho hayo hufanyika katika halmashauri zote nchini kwa ngazi ya Kitaifa .
Mh. Ummy ameogeza kuwa maadhimisho hayo yatafanyika Kitaifa katika Mkoa wa Tanga na kuhusisha shughuli mbalimbali ikiwemo Maonyesho ya teknolojia na kazi za wasioona, upimaji wa elimu na Ujenzi wa wasioona, kongamano la wadau na jamii ya na shughuli za burudani na hotuba na viongozi wa Serikali na wadau.
Mh. Ummmy amezungumza hayo kuelekea maadhimisho ya siku ya Breli nchini yatakayofanyika Mkoani Tanga tarehe 12 February 2026 akiwa na waandishi wa habari katika ukumbi wa ofisi hizo jijini Dodoma leo, akitoa tamko hilo huku kauli mbiu ya Shughuli hiyo ni “Teknolojia ya breli husaidia kuchochea kwa wasioona na ujenzi wa Taifa.”
Nderiananga ameongeza kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za wenye ulemavu hususani wasioona wanapata haki ,fursa na huduma sawa kama wananchi wengine ikiwemo kiuchumi,kijamii,kisiasa na kitamadu hi pia kuwapa sera ya Taifa ya maendeleo ya huduma na mafunzo ya mwaka 2004 sera ya Elimu ya Taifa mafunzo ya 2014 toleo la 2023, sera ya ajira ya mwaka 2008 pamoja na utekelezaji wa sheria ya watu wenye ulemavu.
Kwa upende wake katibu wa chama cha wasioona Mkoa wa Dodoma Enock Mbawa amesema ushiriki wa watu wenye ulemavu unafanya watu wengine waamke kwa kusoma kwa bidii kufanya kazi kwa bidii na kujitoa katika makongamano mbalimbali ambayo ya nahusisha watu wasioona na walemavu wengine mfano Naibu Waziri Nderiananga na kuelekeza pongezi nyingi kwa Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

