Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi katika taasisi mbalimbali za umma, akiwemo Spika mstaafu wa Bunge, Anne Makinda.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatano, Februari 11, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu, imeeleza kuwa uteuzi huo unaanza mara moja.
Katika uteuzi huo, Makinda ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Jaffer Machano ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC), akichukua nafasi ya Ally Karavina.
Naye, Dk Albina Chuwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC).
Katika uteuzi mwingine, Profesa Makena Maboko ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).