Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inashiriki Mkutano wa 48 wa Baraza la Mawaziri Afrika unaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia kuanzia Februari 11-12, 2026. Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.shimiwa Mahmoud Thabit Kombo (Mb).
Mkutano huo unawakutanisha Mawaziri wa Mambo ya Nje na viongozi waandamizi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kujadili masuala muhimu ya maendeleo, usalama, ushirikiano wa kikanda na utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali.
Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), Mhe. Mahmoud Youssouf Ali, amesisitiza umuhimu wa mageuzi ya Taasisi na umuhimu wa amani na maendeleo barani Afrika kuelekea Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU.
Amesema kuwa, Mageuzi yanaendelea chini ya Mpango wa 2024–2028 na kubainisha mafanikio yaliyopatikana katika kuimarisha muundo wa amani na usalama, kuhakikisha ufadhili endelevu, pamoja na kuimarisha taasisi za Umoja huo. Ameishukuru Jamhuri ya Angola kwa uongozi wake wa Baraza la Utendaji, huku Angola ikiwa ni Mwenyekiti wa Umoja huo anayemaliza muda wake.
Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Mhe. Gedion Timothewos, ameeleza kuwa mabadiliko yanayoendelea katika siasa za kimataifa yanazidi kudhoofisha misingi ya ushirikiano wa kimataifa na mfumo wa ushirikiano wa kimataifa.
Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi ya Afrika (UNECA) Mhe.Clever Gatete ameongelea utafutaji fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa nchi wanachama, kuunganisha miundombinu ya uzalishaji, kuongeza thamani ya madini na mazao, kuimarisha soko huru barabi Afrika na kutumia maarifa na teknolojia ya sasa ili kupata maendeleo.
Mkutano huo wa ngazi ya juu wa mawaziri ni sehemu ya maandalizi kwa ajili ya Kikao cha 39 cha Kawaida cha Wakuu wa Nchi na Serikali




