DAWASA Yataka Wananchi Kusubiri Utafiti

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya usimamizi wa maji na safi na taka mkoa wa Dar es salaam (Dawasa) imesema kuwa inaendelea na tafiti katika wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam ili kujua uhitaji wa maji safi na salama kwa wakazi wake.
Mpango huo wa uchimbaji visima mkoa wa Dar es salaam ni kutokana na kukabiliana na upungufu wa maji ili kupunguza umbali wa kufuata maji.
Afisa habari wa mamlaka ya usimamizi wa maji safi na taka mkoa wa Dar es salaam Everlast lyaro amesema kuwa mamlaka hiyo itatoa taarifa pindi kazi hiyo ya utafiti ukimaliza.
Ameongeza kuwa kwa wale ambao pia wanataka kuchimba visima wanaruhusiwa ila wawasiliane na wenye mamlaka ya usimamizi wa maji Bonde la Wami kwa maelezo zaidi.
“mpango upo ila bado tunaendelea na tafiti katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar maeneo ya Mbagala, Chamazi na maeneo yote ya wilaya ya Temeke ili kujua uhitaji na gharama za uchimbaji visima hivyo katika mkoa wa Dar es salaam”amesema Afisa habari Bi Lyaro.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bonde la Mto Wami Ruvu Joseph Mmasi ambao ni wasimamizi wa maji ardhini ameelekeza kuwa Bonde la mto Wami Ruvu ni wasimamizi na wenye mamlaka yote ya maji yaliopo ardhini.
Na kuendelea kusema kuwa kwa kikundi au kampuni wanaotaka kuchimba visima ni lazima wafuate taratibu za Bonde la Mto Wami Ruvu kwa kuwa na viambatanisho vinavyoweza kupatiwa kibali cha uchimbaji.
Aidha Mmasi ameeleza kuwa kwa Kampuni ya uchimbaji lazima iwe imesajilliwa na Wizara ya maji .
” Kwa wenye kikundi au taasisi lazima awe na viambatanisho kadhaa ikiwemo ripoti ya uchumguzi wa sehemu usika ya uchimbaji kisima, barua ya umiliki wa ardhi katika sehemu husika na barua ya utambulisho kutoka kwenye Kijiji au Mtaa” amesema Mmasi.
Uchimbaji wa visima hivyo ni mkakati wa wizara ya maji kwa kushirikiana na Dawasa katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika mkoa wa Dar es salaam.