Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt.Asha-Rose Migiro, leo, Alhamis, Februari 12, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Namibia hapa nchini, Mheshimiwa Gabriel Pandureni Sinimbo.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam.

