Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Dkt Nkunde Mwasaga akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam akitoa taarifa ya kufanyika Tuzo za TEHAMA 2026.
………………
NA MUSSA KHALID
Tume ya TEHAMA nchini (ICTC) kwa kushirikiana na wadau
wa TEHAMA inatarajia kutoa tuzo ya TEHAMA 2026 ikiwa ni kutambua uvumbuzi,
mabadiliko ya kidijitali, na ubora wa TEHAMA unaounda mustakabali wa taifa.
Akizungumza wakati akitambulisha ujio wa Tuzo hizo
jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Dkt Nkundwe Mwasaga
amewataja wadau shiriki kuwa ni pamoja na Chama cha Watoa huduma za Mtandaoni
Tanzania (TISPA) na SophtVenture ambayo ni Kampuni ya Kitanzania
inayoshughulika na ubunifu wa kiteknolojia,maendeleo ya Program na ushauri wa
kidigitali.
Dkt Nkunde amesema kuwa Tuzo hizo zinalenga kutambua
jitihada za kipekee zilzizofanywa na wadau wa TEHAMA na kutia hamasa katika
maeneo mbalimbali ambayo TEHAMA inatumika ikiwemo huduma za
kijamii,uzalishaji,utafiti,ubunifu,utawala na elimu.
Amesema tuzo zitakazotolewa zipo katika makundi mbalimbalki ambapo ni pamoja na Uvumbuzi katika
Bidhaa au Huduma za TEHAMA; Usalama wa TEHAMA – Usalama wa Mtandao na Ulinzi wa
Data; Ubora na Mabadiliko ya Kidijitali; Kijana Mwenye Mafanikio katika TEHAMA;
Wanawake katika TEHAMA; Matumizi Bora ya TEHAMA; TEHAMA katika Utangazaji,
Vyombo vya Habari na Uandaaji wa Maudhui.
Dkt Nkundwe Tuzo ya TEHAMA Endelevu; Tuzo za TISPA kwa
Mtoa Huduma Bora za Mawasiliano; Tuzo za TEHAMA katika Utafiti, Uvumbuzi na
Machapisho; TEHAMA kwa Watanzania waishio Nje ya Nchi (Diaspora); Tuzo za
TEHAMA kwa Maendeleo; pamoja na Tuzo Maalum ya Utambuzi kutoka Wizara ya
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya SoftVenture Solutions
Company Limited ambao ndio waratibu wa tuzo hizo Caroline Kombe amesema lengo
lao ni kusimamia na kuhakikisha uwazi na uadilifu wa mchakato ikiwemo
kusimamiza mawasiliano na uhamasishaji ili kufikia watu wengi zaidi.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Chama cha Watoa
huduma za mitandao nchini (TISPA) Mzee Hamisi Boma amesema wataendelea kuwa
washiriki wakubwa wa TEHAMA ili kuwafikia watumiaji wengi zaidi huku Mkurugenzi
wa Kampuni ya Deloitte na Kiongozi wa Kutoa Ushauri kwa TEHAMA Daniel Materu
akisema lengo lao ni kuhakikisha tuzo hizo zinaendeshwa kwa kuzingatia haki na
uwazi.
Tuzo za TEHAMA ambazo dirisha limefunguliwa hadi tar
15 Machi mwaka huu ni muendelezo wa Tuzo za TEHAMA zilizofanyika kwa mara ya
kwanza 2025 jijini Arusha hivyo wadau mbalimbali wakiwemo wajasiriamali,watoa
huduma pamoja nawawekezaji wametakiwa kutumia fursa ya kushiriki kwenye tuzo
hizo.