Zaidi ya wananchi 7000 wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kunufaika na huduma ya bima ya afya kwa wote kwa awamu hii ya uzinduzi.
Mpango wa bima ya afya kwa wote wazinduliwa katika kijiji cha Kising’a Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Februari 10, 2026.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa tarafa wa tarafa ya Ismani Ndg. Benitho Kayugwa ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Iringa amesema serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania imeona wananchi wake wanavyopata tabu hasa katika sekta ya afya na wameanza na makundi maalumu ambao watapata kadi za bima ya afya ili kupata matibabu bure, huku akiwasisitiza wananchi wanufaika kuzitunza kadi hizo.
Aidha, Wananchi 7827 kutoka halmashauri ya wilaya ya Iringa yenye kata 28 wamashatambuliwa na wanatarajiwa kunufaika na mpango wa bima ya afya kwa wote awamu hii ya uzinduzi.
Kampeni hii inaendelea kwa kata zote za Halmashauri yenye lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma za matibabu pasipo vikwazo vya kifedha.
Kwa upande wake mratibu wa bima ya afya kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Dkt Renatha Kato amesema, Halmashauri ya Wilaya inaanza zoezi hilo kwa awamu ya na kaya zisizokuwa na uwezo, ambazo zitagharamiwa na Serikali.



.jpeg)





.jpeg)
