Russia. Wanaume mara nyingi hulala usingizi mzito baada ya kushiriki tendo la ndoa, na hii ni kutokana na kutiririshwa kwa vichochezi mchanganyiko baada ya kufika kilele.
Kupata hali ya usingizi mzito sio tatizo la kiafya, bali ni hali ya kawaida ya kiasili ya ufanyaji kazi za mwili baada kufika kileleni, ambapo huleta usingizi mzito ili kuupa nafasi mwili kurudi upya au kupona.
Usingizi mzito huchangiwa na michakato mingi ikiwamo mabadiliko mfumo wa fahamu, vichochezi, kupungua kwa nguvu, kushuka kwa shinikizo na utilivu wa mwili.
Kibailojia Wanaume ndio wanaopata usingizi mzito hii ni kutokana na mwanaume kuwa na kiwango kikubwa cha kichochezi cha Prolactin kuliko wanawake. Kichochezi hiki ndicho humfanya mtu kutosheka na tendo hatimaye hali ya usingizi.
Kupata usingizi huwa na faida kiafya kwani hapa mwili huweza kupona hatimaye baadaye tena kufanya majukumu mengine. Ndio maana hata wenye tatizo la usingizi hushauriwa kufanya tendo hili.
Ikumbukwe kuwa hitajio la mwili kulala huwa ni ishara kuwa mwili unahitaji kujikita zaidi na kazi za ndani ya mwili, unapolala mwili unazima mawasiliano ya nje. Jambo hili linaupa mwili nafasi ya kupona.
Baada ya mwanaume kufika kileleni homoni za plolactin na oxytocin hutolewa ambazo husababisha hali ya utulivu, kupunguza wasiwasi na kuleta usingizi.
Tendo hili linachukua nafasi kubwa ya mfumo wa fahamu usio wa hiari. Zaidi ya hayo mwili hurudi katika hali ya chini kimhemko na tendo hili hutumia nguvu ambayo nayo hushuka baada ya nishati kutumika hatimaye huhitaji kulala ili kupata uponaji.
Mifumo miwili ya fahamu isiyo ya hiari hubadilishana, baada ya tendo mwili hurudi katika mfumo wa kushusha mihemko usio wa hiari ili kuruhusu mwili kurudi katika ya hali ya asili ya kupona.
Kiwango cha kichochezi cha prolactin kuongezeka baada ya kufika kilelen na ndio huchangia usingizi na hali ya kuridhika. Kipindi hiki mwili hushusha hamu ya tendo ili kujipa muda wa kupona.
Vile vile kuna vichochezi burudisho vinavyotolewa ambavyo ni Serotonin na Oxtosin, hivi huleta hali ya furaha, utulivu mkubwa, kushusha msongo wa mawazo na kuuongeza hali ya kuburudika hatimaye usingizi.
Tendo la ndoa huwa na harakati nyingi zinazoufanya mwili kushughulisha viungo vingi na huku ikitumia nguvu nyingi hivyo kushusha kiwango cha nishati iliyohifadhiwa katika misuli na kuleta mchoko.
Na kwa sababu wanaume huwa na misuli mikakamavu zaidi yenye kutumia nguvu zaidi, kupungua kwa nishati kunaufanya mwili kupata mchoko hivyo kuhitaji uponaji kupitia usingizi.
Ubongo ambao ndio mdhibiti mkuu hupata utulivu mkubwa wakati wa kufika kileleni, kwasababu ya kuzuiwa kichochezi kijulikanacho kama Cortisol ambacho huleta shinikizo mwilini.
Mambo haya ni mwitikio wa asili wa mwili, wanawake kwa wanaume wote hupata usingizi baada ya kufika kileleni, lakini kwa mwanaume ni zaidi kwa sababu za kimaumbo na za kibailojia.