Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa Kagera kanali Yahaya Ramadhani Kido amesema suala la ulinzi na usalama litakuwa kipaumbele chake cha kwanza kutokana na mkoa huo una mipaka yenye uingiliano mkubwa na nchi jirani.
Katika hafla fupi ya hati ya makabidhiano kati yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatma Mwassa ,Kanali Kido amesema suala la ulinzi na usalama wa nchi sio la kubembelezana isipokuwa Kila mtanazania anapaswa kutoa taarifa haraka pale anapomtilia mashaka mgeni yeyote anayeingia nchini bila kibari.
“Kagera ni mkoa wa kimkakati nyote mtakuwa mlisikia maagizo ya Mheshimiwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuhusu ulinzi na usalama hivyo naomba vyombo vya usalama tuchukue hatua kukabiliana na wimbi la wahamihaji wanaokimbilia katika mkoa huu kufuga ,kulima kujimilikisha,hii nchi ni yetu na sio Mali ya wageni kutoka nje “amesema.
Aidha amesema pia kipaumbele chake cha pili ni kuhakikisha miradi ya kimkakati yote inatekelezwa na kukamilika kwa wakati kwani miradi hiyo ndio yenye kuchochea Uchumi kwa wananchi.
“Miradi inayotekelezwa katika halmashauri lazima iendane thamani ya fedha na ikamilike ili kusogeza huduma Bora kwa wananchi wa mkoa wa Kagera.”
Awali kabla ya makabidhiano aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Fatma Mwassa amesema Mkoa wa Kagera unakabiliwa na changamoto ya wahamihaji kutoka nchi za Burundi,Rwanda,Uganda na nchi nyingine za Sudan Na congo
Amesema kwa mwaka 2024 hadi Novemba 2025 wahamihaji haramu walioingia nchini na kurudishwa walikuwa 17,200 na kati ya hao asilimia 85,ilitoka Burundi ,asilimia 5 Rwanda ,asilimia 5 Uganda na asilimia Nyinginezo .
“İdadi hiyo ni kubwa sana na inahitaji kuchukua hatua za haraka na weledi mkubwa kwani wengi ufata aridhi marisho na vibarua na baadhi wakifika wanaoa na kuolewa.”
Pia amesema mkoa huo unamiradi mingi inayotekelezwa huku akitaja kuwa uchumi wa Kagera kwa miaka mingi umekwama kutokana na kutokuwa na maamuzi ya kuwaweka vijana katika mpango mkakati wa kuwapatia kipato cha mwaka mzima kupitia sekta za kilimo mifugo na uvuvi na wengi wakitegemea ajira kutoka serikalini.
Fatma Mwassa amewashukuru wananchi na viongozi kwa ushirikiano na mipango thabiti ya kuendeleza mkoa huo ikiwemo mpango mkakati wa kuwapatia ajira vijana 2,000 Kila halmashauri kupitia Sekta ya kilimo ,mifugo,uvuvi na viwanda.



