TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imeendelea na vikao vyake leo Februari 16, 2026 kwa kukutana na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Faraji Mnyepe na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ally Gugu.
Mkutano huo wa Tume na Makatibu Wakuu hao umefanyika katika ukumbi wa Tanganyika uliopo jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani hapa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Tume kukusanya taarifa, maoni na ushauri kutoka kwa viongozi mbalimbali.
Katika mkutano huo hoja zilizojadiliwa zilihusu maeneo ya tathmini ya athari za matukio hayo na ushauri wa hatua za kijamii na kisheria zinazoweza kuchukuliwa ili kuimarisha amani na mshikamano wa kitaifa.
Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali ikiwemo waathirika wa matukio ya uvunjifu wa amani katika mikoa tofauti nchini, kwa lengo la kukusanya ushahidi na taarifa zitakazoiwezesha kuandaa ripoti ya kina.
.jpeg)
.jpeg)


