MIKOA NANE KUNYESHA MVUA KUBWA KESHO

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Nchini imetoa tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe, Mbeya na Ruvuma.

Mvua hiyo inatarajiwa kunyesha kesho Jumanne Februari 17 2026 katika baadhi yamaeneo ya mikoa hiyo.

Kwa mujibu wa utabiri wa matarajio ya hali mbaya ya hewa uliotolewa na Mamlaka ya Hall ya hewa nchini TMA ni kuwa uwezekano wa mvua hiyo kunyesha ni mkubwa na kwamba watu wanatakiwa kuchukua tahadhari il kujlepusha na madhara yanayoweza kujitokeza.

Taarifa hiyo inazitaka mamlaka za kisekta ikiwemo za afya, elimu, miundombinu, elimu, maji, kilimo, mifugo na hata usafirishaji majini kuchukua tahadhari hasa katika maeneo ambayo mafuruko yanaweza kuchukulivwa.

Mvua hizo zinanyesha ikiwa zimepita siku 11 tu tangu TMA itoe utabiri wa mvua za msimu wa masika katika mikoa inayopata msimu wa mvua mara moja kwa mwaka ambao unaonesha maeneo mengi ya nchi yatapata mvua za wastani hadi juu ya wastanıi.