Kigoma. Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi amewataka viongozi wa Serikali waliopewa dhamana kuacha fitina na chuki, badala yake watimize majukumu ili kufikia malengo ya kuwahudumia Watanzania.
Kihongosi amehimiza uhusiano mzuri kwa watendaji wa Serikali katika maeneo ya kazi, akisema viongozi wakishikamana kushirikiana, kuacha chuki, fitina, husuda na uongo watafanikiwa.
Ameeleza hayo leo Jumatano Februari 18, 2026 wakati akizungumza muda mfupi baada ya kukagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma katika mwendelezo wa ziara yake akitokea Mkoa wa Tabora.
“Viongozi mkiendekeza migogoro, majungu, kushughulikiana mtaharibu kazi, kumbukeni kazi hizi ni wito wa Mungu ametupatia katika nyakati hizi. Kazi tunazozifanya kila mtu anaweza kuzifanya, lakini mmepata fursa za kuzitumikia.
“Wajibu wetu ni kufanya kazi kwa bidii, kwa hiyo mambo ambayo yanayoweza kutugawa na kutuharibia tuyaache badala yake tuangalie kazi,” amesema Kihongosi.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi amewataka viongozi wa Serikali waliopewa dhamana kuacha fitina na chuki, badala yake watimize majukumu ili kufikia malengo ya kuwahudumia Watanzania.
Mbali na hilo, Kihongosi amesema CCM imeridhishwa na ujenzi wa hospitali iliyokamilika na kuanza na kutoa huduma kwa wananchi wa Uvinza ambapo kuna mashine na vifaa tiba vya kisasa.
Katika hatua nyingine Kihongosi amewapongeza watumishi wa hospitali hiyo kwa moyo wa kizalendo wa kutoa huduma akiwaomba wananchi wa wilaya hiyo kuwatia moyo na kuwaunga mkono.
Awali, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Dk Maira Biseko amemweleza Kihongosi hospitali hiyo yenye thamani ya Sh5 bilioni kwa sasa inatoa huduma mbalimbali za wagonjwa wa nje na ndani, maabara, mionzi, uzazi salama na huduma za kuhifadhi maiti.
Dk Biseko amesema uwepo wa hospitali hiyo umewezesha kupungua kwa rufaa za watoto wachanga wanaopata changamoto za kiafya wakiwemo wanaozaliwa na uzito pungufu ‘ njiti’ kwenda Hospitali ya Rufaa ya Maweni mkoani hapa.
“Jamii inanufaika na huduma zinazotolewa hapa ambazo zimewapunguzia umbali na muda wa kufuata huduma za afya katika Hospitali ya Maweni,” amesema Dk Biseko.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi amewataka viongozi wa Serikali waliopewa dhamana kuacha fitina na chuki, badala yake watimize majukumu ili kufikia malengo ya kuwahudumia Watanzania.
Hata hivyo, Dk Biseko amesema hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa watumishi, nyumba za watumishi hatua inayosababisha kuishi mbalimbali na kituo chao cha kazi.
Kutokana na hilo, Kihongosi amemweleza Dk Biseko kuwa ajira mpya za watumishi wa kada ya afya 5,000 zilizotolewa na Serikali, baadhi yao watazingatiwa kwenda katika hospitali hiyo.