Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akishiriki Ibada ya Jumatano ya Majivu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu, Paul wa Msalaba Jimbo Kuu Katoliki Dodoma leo tarehe 18 Februari 2026. Ibada ya Jumatano ya Majivu ni mwanzo wa kipindi cha Kwaresma ambacho hutumika na waumini wa dini ya Kikristo kwaajili ya mfungo.MAKAMU Nchimbi ameungana na waumini mbalimbali kushiriki Ibada ya Jumatano ya Majivu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu, Paulo wa Msalaba Jimbo Kuu Katoliki Dodoma leo tarehe 18 Februari 2026.
Ibada hiyo, imeongozwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma Wilbroad Kibozi.
Akitoa mahubiri katika Ibada hiyo, Askofu Kibozi, amewasihi waamini kutumia kipindi hiki cha mfungo wa Kwaresma, kujitoa kwaajili ya wahitaji pamoja na kuombea familia, vijana, watoto na Taifa kwa ujumla.
Pia amesema katika kipindi hiki ambacho waumini wa Dini ya Kikristo na Kiislamu wanakutana pamoja katika mfungo, ni vema kupendana, kuheshimiana na kujaliana.
Askofu Kibozi amesema wafanyabiashara wanapaswa kuwa wema na wakarimu katika kipindi hiki na kutambua kipindi hiki sio cha upandishaji bei ya bidhaa za vyakula bali inapaswa bei za bidhaa kupunguzwa.
Ibada ya Jumatano ya Majivu ni mwanzo wa kipindi cha Kwaresma ambacho hutumika na waumini wa Dini ya Kikristo kwaajili ya mfungo.
