Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir amethibitisha taarifa ya kuandama kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Amewaambia waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam kuwa, kufuatia kuandama kwa Mwezi Mtukufu, Waumini wa dini ya Kiislam katika maeneo mbalimbali nchini wataanza Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan hapo kesho Febuari 19 2026
Mufti wa Tanzania amesema Mwezi umeonekana katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Kenya.
Related
