YASSIN: SIKU 100 ZA RAIS SAMIA ZIMELETA MWANGA WA MAENDELEO TANZANIA

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Daud Yassin amesema siku 100 tangu kuingia madarakani kwa Rais, Dkt Samia zimekuwa na mwanga mkubwa wa kuleta maendeleo nchini.

Amesema kazi nyingi zimeendelea kutekelezwa huku changamoto za Watanzania zikitatuliwa kupitia sekta zote.

Akizungumza katika taarifa yake kupitia mitandao ya kijamii, Yassin amesema amani na utulivu vimeifanya Tanzania kuendelea kung’aa zaidi.

“Siku 100 za Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan zimekuwa zenye mwanga mkubwa wa maendeleo katika nchi yetu,” amesema Yassin.

Yassin amesema anaungana na Watanzania wote kumtakia heri Dkt Samia na viongozi wote katika utekelezaji wa majumu yao.