TFF Yataka Kampuni Moja Pekee ya Kubashiri – Global Publishers



SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwa linatafuta kampuni moja kwa ajili ya haki za kipekee za ubashiri (exclusive betting rights) katika mechi ya Yanga na Simba utakaochezwa Machi 01, 2026 katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia saa 2.15 usiku.

Kupitia taarifa yake ya leo Februari 18, 2026, TFF imewakumbusha wadau wote wa michezo ya kubashiri kuwa haki zote za Ligi Kuu ya NBC ni mali ya TFF na washirika wake (partners) na kusisitiza kuwa kampuni yoyote itakayobashiri mechi hiyo na nyingine ambazo ni mali ya TFF itachukuliwa hatua kali za kisheria.