RAIS MWINYI KUONGOZA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA QUR’AN DAR ES SALAAM

:::::::

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Mashindano Makubwa ya Kimataifa ya Qur’an Tukufu yatakayofanyika Jumapili, Machi 1, 2026.

Katika mashindano hayo, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwa Mgeni Maalum. Tukio hilo linasimamiwa na Alhikma Foundation.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya taasisi hiyo yaliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya mashindano hayo, Sheikh Nurdeen Kishk, alisema maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa.

Alisema kutokana na mabadiliko ya majira, mashindano hayo yataanza saa 12:15 asubuhi.

Mashindano hayo yatafanyika katika Viwanja vya Benjamin Mkapa Stadium, jijini Dar es Salaam.

Sheikh Kishk alieleza kuwa lengo la kuanza mapema ni kutoa fursa kwa waumini na wadau wengi zaidi kushiriki tukio hilo muhimu la kidini.