Dodoma Jiji Waisimamisha Simba Watoka Sare, Macho Yote Yanga vs Simba

Global Publishers
February 26, 2026
0 Comments

Simba wameshindwa kufurukuta katika dimba la Jamhuri, Dodoma baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana (0-0) dhidi ya Dodoma Jiji FC maarufu kama Wakulima wa Zabibu.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba walimiliki sehemu kubwa ya mchezo lakini walikosa makali ya kumalizia nafasi walizozitengeneza. Dodoma Jiji kwa upande wao walionyesha nidhamu ya hali ya juu katika safu ya ulinzi, wakihakikisha wanaondoka na alama moja muhimu nyumbani.

Matokeo hayo ni pigo kwa Simba katika mbio za ubingwa, hasa ikizingatiwa ushindani mkali uliopo msimu huu.

Baada ya matokeo hayo, kituo kinachofuata ni dimba la New Amaan Complex visiwani Zanzibar, maarufu kwa jina la utani Guantanamo Bay, ambapo itapigwa Kariakoo Derby  kati ya wenyeji Yanga dhidi ya Simba.

Mchezo huo utakaochezwa Machi 01, 2026 unatarajiwa kuwa na presha kubwa, ushindani mkali na historia ya kipekee, hasa baada ya Simba kupoteza pointi muhimu Dodoma.

Yanga wataingia dimbani wakisaka kuendeleza ubabe wao au kupunguza presha ya mbio za ubingwa, huku Simba wakihitaji ushindi ili kufuta majonzi ya sare ya Dodoma.