Kifo cha Baba Kimeacha Pengo Kwa Mtoto Mlemavu, Mama Afunguka – Video

Global Publishers
February 26, 2026
0 Comments

Ni siku ya pili sasa tangu kufanyika kwa mazishi ya marehemu Yohana Kamingwe, baba mzazi wa mtoto Gidion mwenye ulemavu wa mikono, mkazi wa Temeke Mtoni Unguja.

Marehemu Yohana Kamingwe alizikwa juzi katika makaburi ya Site Yombo Dovya majira ya saa kumi, huku ndugu, jamaa na wakazi wa maeneo ya jirani wakijitokeza kumpa heshima za mwisho.

Gidion, ambaye alikuwa akipata msaada mkubwa kutoka kwa baba yake mzazi, sasa amebaki mikononi mwa jamii baada ya mlinzi wake mkuu kutangulia mbele ya haki. Kifo cha baba huyo kimeacha pengo kubwa katika maisha ya mtoto huyo, hususan kutokana na hali yake ya ulemavu inayohitaji uangalizi na msaada wa karibu.

Wananchi wenye moyo wa kusaidia wameombwa kujitokeza kumuunga mkono Gidion ili aweze kuendelea na maisha pamoja na kupata mahitaji muhimu ya kila siku.

📞 Namba ya msaada: +255 773 224 779 Jina: Yohana Gilayo

Msaada wowote, mkubwa au mdogo, unaweza kuwa tumaini jipya kwa maisha ya mtoto huyu.

Video full ipo YouTube ya Global T
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.