Masaju akomaa na haki za raia

Dar es Salaam. Wakati Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju, akiwataka majaji na mahakimu kuhakikisha wanatenda haki, kuzingatia maadili na kujiepusha na vitendo vya rushwa, wadau wamesema azma hiyo itafanikiwa iwapo wahusika watatengenezewa mazingira mazuri ya kazi.

Aidha, mkuu huyo wa muhimili wa Mahakama amewaeleza watendaji hao kutekeleza majukumu yao bila kusubiri au kufuata maelekezo, akisema: “Maelekezo yataharibu mahusiano tuliyonayo; maelekezo yana tabia ya uelekezaji, hivyo kila mtu awajibike ipasavyo.”

Masaju amesema hayo kwa nyakati tofauti jijini Dodoma—Februari 23, 2026 alipokuwa akiwaapisha mahakimu wakazi wapya 90 wa mahakama ya mwanzo, na Februari 25, 2026 alipokuwa akifungua kikao cha kwanza cha majaji wafadhiwi wa Mahakama Kuu.

“Ninyi ambao mmeapishwa leo hamkuapa mbele yangu mimi; mliapa kwa Mwenyezi Mungu. Nimeona mmebeba vitabu—wengine Biblia, wengine Qur’an Tukufu. Mlivyokuwa mnaapa sikusikia mkisema ‘Ee Jaji Mkuu nisaidie.’ Kila mmoja amesema ‘Ee Mwenyezi Mungu nisaidie.’

“Kwa kadri mlivyokula viapo hivyo, njooni mviishi. Maneno mliyoyaapa yapo katika Ibara ya 107A (1) pamoja na ibara ndogo ya kwanza na ya pili (a) na (b), lakini yapo pia katika Ibara ya 107B. Nendeni mkayaishi,” amesema Masaju.

Akisisitiza hilo, amesema dhamana ya utoaji haki ni jukumu zito linalohitaji nidhamu, uaminifu na weledi wa hali ya juu.

 Ameeleza kuwa mahakimu wanapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya sheria, kuepuka upendeleo na kuhakikisha wanawatendea wengine yale wanayotamani wenyewe watendewe.

Kwa mujibu wa Masaju, asilimia 70 ya mashauri yaliyopo mahakamani yako katika mahakama ya mwanzo, hivyo mahakimu wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha haki inatendeka.

Kuhusu uadilifu, amewataka mahakimu kutopokea wala kutoa rushwa, akisema rushwa huchangia kwa kiasi kikubwa kuporomosha maadili ya utumishi. Ameongeza kuwa sifa kuu ya hakimu inapaswa kuwa unyenyekevu.

Amesema kadri mtu anavyokuwa na madaraka makubwa ndivyo kiwango chake cha unyenyekevu kinapaswa kuongezeka, ili wawe watumishi wa watu wote.

Jaji Mkuu huyo ameweka wazi kuwa watumishi wanapaswa kuwa mfano kwa wengine kwa kuishi kiapo cha maadili ya kazi.

Ameonya kuwa yeyote atakayekiuka maadili na sheria za kazi, Mahakama haitasita kumchukulia hatua za kisheria na kumwajibisha.

Ameongeza kuwa sifa ya mahakama huharibika pale watumishi wanapokiuka maadili ya utumishi na kushiriki vitendo vya rushwa, akisisitiza Serikali inawatazama, Mungu pia anawatazama.

Amesema Mahakama ni mhimili muhimu wa dola unaosimamia haki na kudumisha amani katika jamii; hivyo kila hakimu ana wajibu wa kulinda heshima, hadhi na taswira ya Mahakama mbele ya wananchi.

Jaji Mkuu amewashauri mahakimu kutoruhusu Mahakama kutumiwa vibaya, kutokubali maahirisho ya kesi yasiyo na msingi na kuhakikisha mashauri yaliyo mbele yao yanahitimishwa mapema ipasavyo kwa kuzingatia sheria.

Katika mkutano wa majaji wafawidhi, Masaju amesema inapaswa kuwa ya mfano na kimbilio la kila mtu na kuwa hata yeye akitenda kosa atapelekwa mahakamani, hivyo ni lazima wao wawe mfano.

“Nataka tuone taswira ya Mahakama kuanzia mahakama ya mwanzo na rufani, watu wanaona mahakama ya mwanzo ni kitu gani, wanaona mahakama ya rufani ni kitu gani,” amesema.

“Sisi huku tulipo tutaendelea kuwahimiza tufikie kiwango cha kudumisha heshima, uhuru na mamlaka ya mahakama ambao umelindwa kikatiba katika ibara ya 30(2) d.

Amesema wasipofanya hayo watu wengine watajitokeza kufanya na wataanza kulalamika kuingiliwa, jambo ambalo wao wenyewe ndio watakuwa wameyakaribisha.

 “Akili ya kwamba tunazungumza hapa wanaohusika hawatekelezi wanasubiri kikao kingine, hatutakuwa na utamaduni wa aina hiyo,” alionya.

Masaju amesema kushughulikia haraka changamoto kutasaidia kuwezesha hatua za haraka kuchukuliwa na kupunguza mrundikano.

“Tujenge utamaduni wa kuzishughulikia changamoto haraka pale zinapojitokeza, tusiziendekeze, we zishughulikie lakini zikikushinda zipandishe ngazi husika.

Jaji mkuu ametaka mashauri ya mirathi yapewe kipaumbele na ndio maana wameyatungia kanuni.

“Tunahimiza mashauri ya mirathi muyape kipaumbele, yanayohusu wanawake na watoto, hawa sio dhaifu ila baadhi ya jamii inawaona hivyo, ndio maana baadhi wanapoteza haki zao, mjane ana uchungu wa kufiwa na mumewe na hawezi kujieleza,” amesema.

Mchambuzi wa Masuala ya siasa, Magabilo Masambu amesema agizo hilo la Jaji Mkuu limeweka msisitizo muhimu juu ya uwajibikaji, uadilifu na ufanisi ndani ya mhimili wa mahakama.

“Anapowataka majaji wafawidhi kutumia kikamilifu kanuni zilizopo na kushughulikia changamoto mapema, anagusa moja kwa moja tatizo la ucheleweshaji wa haki ambalo limekuwa likilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu.Hii ni hatua chanya inayolenga kurejesha imani ya umma kwa chombo hicho cha utoaji haki,” amesema.

Katika hatua nyingine, Jaji Mkuu Masaju amewaeleza majaji hao wanapokwenda kutumika katika mikoa mbalimbali nchini waelewe mila na desturi za wananchi eneo walipo kwani ndio njia ya kujenga mahusiano nao.

Amesema hata wakoloni walipokuwa wakitoa hukumu walitafakari wananchi wa jamii ile wanafikiri namna gani.

“Ukienda pale sio unasema hawa watu wa Musoma akili zao sio nzuri unajifungui tu ofisini,” amesema.

Jaji Mkuu amesema Mahakama itaendelea kuheshimika kama majaji wataishi viapo vyao na kutekeleza kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi.

Amesema utekelezaji wa hayo ndio utasaidia uhuru wa mahakama kuheshimika na hayo yasipotekelezwa basi watabaki kuitwa wahehimiwa.

Kuhusu maadili, Jaji Mkuu amewaeleza majaji hao kama hawatasimamia vyema eneo la maadili, mabadiliko wanayokusudia kuyafanya yanaweza kutafsiriwa wamelenga kufichiana mabaya na udhaifu wao.

“Februari 2, Rais Samia alituelekeza tusitumie vibaya uhuru wetu wa mahakama kuwa kichana hcha kufichiana madhaifu na rushwa,”amesema.

Katika mkutano wa Majaji Wafawidhi, Masaju amesema: “Akili ya kwamba tunazungumza hapa wanaohusika hawatekelezi wanasubiri kikao kingine hatutakuwa na utamaduni wa aina hiyo.”

Masaju amesema mahakama inapaswa kuwa ya mfano na kimbilio la kila mtu na hata yeye akitenda kosa atapelekwa mahakamani hivyo ni lazima wao kuwa mfano.

“Juzi niwaapisha mahakimu wengine 90, nataka tuone taswira ya mahakama kuanzia mahakama ya mwanzo na Rufani, watu wanaona mahakama ya mwanzo ni kitu gani, wanaona mahakama ya rufani,” amesema.

“Sisi huku tulipo tutaendelea kuwahimiza tufikie kiwango cha kudumisha heshima, uhuru na mamlaka ya mahakama ambao umelindwa Kikatiba Ibara ya 30(2) d.

Amesema wasipofanya hayo watu wengine watajitokeza kufanya na wataanza kulalamika kuingiliwa jambo ambalo wao wenyewe ndio watakuwa wameyakaribisha.

Masaju amesema kushughulikia haraka changamoto itasaidia kuwezesha hatua za haraka kuchukuliwa na kupunguza mrundikano.

“Tujenge utamaduni wa kuzishughulikia changamoto haraka pale zinapojitokeza, tusiziendekeze, we zishughulikie lakini zikikushinda ‘ziescalate’ zipandishe ngazi husika.

Jaji mkuu ametaka mashauri ya mirathi yapewe kipaumbele ndio maana wameyatungia kanuni.

“Tunahimiza mashauri ya mirathi muyape kipaumbele, yanayohusu wanawake na watoto, hawa sio dhaifu ila baadhi ya jamii inanaona hivyo, ndio maana baadhi wanapoteza haki zao, mjane ana uchungungu wa kufiwa na mumewe mtoto hawezi kujieleza,” amesema.

Mchambuzi wa Masuala ya siasa, Magabilo Masambu amesema agizo hilo la Jaji Mkuu limeweka msisitizo muhimu juu ya uwajibikaji, uadilifu na ufanisi ndani ya mhimili wa mahakama.

“Anapowataka majaji wafawidhi kutumia kikamilifu kanuni zilizopo na kushughulikia changamoto mapema, anagusa moja kwa moja tatizo la ucheleweshaji wa haki ambalo limekuwa likilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu.Hii ni hatua chanya inayolenga kurejesha imani ya umma kwa chombo hicho cha utoaji haki,” amesema.

Katika hatua nyingine, Jaji Mkuu Masaju amewaeleza majaji hao wanapokwenda kutumika katika mikoa mbalimbali nchini waelewe mila na desturi za wananchi eneo walipo kwani ndio njia ya kujenga mahusiano nao.

Amesema hata wakoloni walipokuwa wakitoa hukumu walitafakari wananchi wa jamii ile wanafikiri namna gani.

“Ukienda pale sio unasema hawa watu wa Musoma akili zao sio nzuri unajifungui tu ofisini,” amesema.

Jaji Mkuu amesema Mahakama itaendelea kuheshimika kama majaji wataishi viapo vyao na kutekeleza kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi.

Amesema utekelezaji wa hayo ndio utasaidia uhuru wa mahakama kuheshimika na hayo yasipotekelezwa basi watabaki kuitwa wahehimiwa.

Kuhusu maadili, Jaji Mkuu amewaeleza majaji hao kama hawatasimamia vyema eneo la maadili, mabadiliko wanayokusudia kuyafanya yanaweza kutafsiriwa wamelenga kufichiana mabaya na udhaifu wao.

“Februari 2, Rais Samia alituelekeza tusitumie vibaya uhuru wetu wa mahakama kuwa kichana hcha kufichiana madhaifu na rushwa,”amesema.

Kauli ya Jaji Mkuu pia amewaonya majaji wafadhi kutoishi kwa maelekezo

“Hatuwezi kuishi kwa maelekezo, maelekezo yataraharibu mahusiano tuliyonayo, maelekezo yanatabia ya uelekezaji hivyo kila mtu awajibike ipasavyo.

“Akili ya kwamba tunazungumza hapa wanaohusika hawatekelezi wanasubiri kikao kingine hatutakuwa na utamaduni wa aina hiyo” amesema.

Masaju amesema mahakama inapaswa kuwa ya mfano na kimbilio la kila mtu na hata yeye akitenda kosa atapelekwa mahakamani hivyo ni lazima wao kuwa mfano.

Amesisitiza mafanikio ni lazima yawe yamechangiwa na kila mtu na hayawezi kuwa na msukumo kutoka kwa mtu mmoja.

“Tunataka mafanikio yanayokuwa ‘genereted’ yanayotengenezwa na kila mmoja wetu kwenye muhimbili huu au taasisi hii, tusiishi maelekezo maelekezo sijui yanatoka wapi…?” amesema

Jaji huyo ametoa kauli hiyo akikumbusha hotuba yake aliyoitoa wakati akizungumza na wasajili Desemba 2025, akisema hawawezi kuishi kwa maelekezo kwani wao ni binadamu na wana akili kuliko wanyama.

Katika hilo, amesema wanapaswa kutambua wajibu wao na kwamba binadamu ili aendelee kimwili, kiroho na kiakili anapaswa kujua anafanya nini na kuchukua hatua.

‘Atengeneze mazingira’

Akizungumzia kauli hiyo, Mchambuzi wa masuala ya siasa, Dk Paul Loisulie amesema kauli ya Jaji Mkuu ni nzuri lakini anapaswa kwenda mbali zaidi kwa kutengeneza mazingira bora ya majaji kufanya kazi.

Dk Loisulie amesema maelekezo hayatakuwepo endapo mazingira ya majaji yatakuwa mazuri.

“Kumekuwa na malalamiko ya wadau wa masuala ya sheria na haki na Jaji Mkuu anafahamu ni nini wanacholalamikia watu hao, badala ya kurusha lawama atengeneze mazingira ya utendaji kazi,” amesema.

Mchambuzi huyo amedai mahakama inafanya kazi katika mazingira ya kisiasa na hata majaji upatikanaji wao ni wa kisiasa hivyo ni ngumu watendaji kufanya kazi nje ya mfumo wa kisiasa.

Amesema mazingira ya kisiasa yanapokuwa mazuri hata utendaji wa majaji nao utakuwa mzuri lakini ukiwa mbaya lazima utendaji wao uathirike.

Kwa upande wake, Mwalimu Samson Sombi amesema, suala la kupewa maelekezo si jambo baya lakini ni kwanini mtumishi wa Serikali aliyeajiriwa kwa taaluma yake kusubiri apewe maelekezo.

“Kila mtu afanye kazi kulingana na taalamu yake, kwanini usubiri maelekezo wapo watumishi wengine wanatumia mwanya huo kuumiza wengine, anafanya jambo anasema ni maelekezo amepokea,”amesema.

Amesema neno maelekezo limekuwa kichaka cha kujificha kwa baadhi ya watumishi kutenda mambo yasiyo sahihi ambayo matokeo yake ni kuichonganisha Serikali na wananchi.

Mwalimu Sombi amesema mtu anapopewa maelekezo ya jambo lolote ndani ya taaluma yake, anapaswa kutumia akili yake kuchangua usahihi wa maelekezo hayo kabla ya kuanza utekelezaji.

Mchambuzi wa Masuala ya Siasa, Tumaini Mnale kwa upande wake amesema kauli ya Jaji Mkuu ni wito muhimu katika kuimarisha misingi ya haki na utawala wa sheria nchini.

Amesema kauli hiyo inakuja wakati jamii ikiendelea kuwa na matarajio makubwa kwa mhimili wa Mahakama kusimamia haki bila upendeleo wala shinikizo la aina yoyote.

“Maadili katika utoaji wa haki si jambo la hiari bali ni wajibu wa kikatiba na kiutumishi. Jaji au hakimu anapozingatia uadilifu, anaimarisha imani ya wananchi kwa Mahakama na kulinda hadhi ya taaluma ya sheria.

Kinyume chake, vitendo vya rushwa au upendeleo huondoa taswira ya chombo hicho na kuathiri haki za watu wasio na sauti,” amesema.

Aidha, Munale amesema kauli hiyo ni ujumbe kwa watendaji wa Mahakama kutambua kuwa wanabeba dhamana ya maisha na mustakabali wa watu kupitia maamuzi yao.