Bakari Mahundu
February 26, 2026
0 Comments
Mkurugenzi wa Global Publishers na Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo, amekabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa vituo vya kulelea watoto yatima na watu wasiojiweza.
Hatua hiyo ni muendelezo wa mpango wa kila mwaka wa kusaidia makundi maalumu, unaotekelezwa kwa kushirikiana na Talib Hillal wa Oman kupitia Maryam Bint Amran Foundation pamoja na Global Publishers.

Misaada hiyo imelenga kuwafariji na kuwasaidia wenye uhitaji, hususan katika kipindi cha mfungo wa Ramadhan. Kwa zaidi ya miaka mitano sasa, Global Publishers kwa kushirikiana na Talib Hillal kupitia Maryam Bint Amran Foundation wamekuwa wakitoa misaada kwa vituo mbalimbali vya yatima na watu wenye mahitaji maalumu nchini.