Live: Rais Dkt. Samia Ashiriki Ibada Ya Kuaga Mwili Wa Kardinali Pengo

Global Publishers
February 27, 2026
0 Comments

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Pengo, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, jijini Dar es Salaam, tarehe 27 Februari 2026.

Rais Samia alijiunga na mamia ya waumini, viongozi wa dini na serikali kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki aliyelitumikia taifa kwa uadilifu na mchango mkubwa wa kiroho na kijamii.

Ibada hiyo maalum iliambatana na sala, nyimbo za maombolezo na tafakari ya maisha na utumishi wa Kardinali Pengo katika kuliongoza Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Kanisa kwa ujumla.