Dar es Salaam. Waombolezaji na waumini, waliojitokeza katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu kwa ajili ya kuuga mwili wa Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, leo Februari 27, 2026.
Wananchi wakiaga mwili wa Kardinali Pengo kanisani
Kardinali Pengo alifariki dunia Februari 19, 2026, katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Misa ya kuuaga itaanza saa 10:00 jioni katika kanisa hilo.
Mwili huo unatarajiwa kuzikwa ndani ya Kanisa la Hija ya Bikira Maria, Pugu kesho Februari 28, 2026 na misa ya mazishi itaanzia saa 4:00 asubuhi.