Global Publishers
February 27, 2026
0 Comments
Mwili wa Marehemu Mwadhama Polycarp Pengo ulivyowasili katika viunga vya Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu – Jimbo Kuu la Dar es Salaam, kutoka Hospitali ya Lugalo Hospital, jijini humo.
Mwadhama Kardinali Pengo, aliyejulikana kwa mchango wake mkubwa katika Kanisa Katoliki na jamii ya Tanzania kwa ujumla, alifariki dunia Februari 19, 2026, alipokuwa akipatiwa matibabu katika Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI).
Mazishi yake yamepangwa kufanyika Jumamosi, Februari 28, 2026, katika Kituo cha Hija Pugu, Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Tarehe hii inatarajiwa kuwa tukio kubwa la maombolezo, ambapo waumini, viongozi wa dini na serikali wataungana kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi aliyehudumia Kanisa kwa moyo wa dhati.

Msafara wa heshima unaonyesha hofu, heshima na simanzi ya waumini waliokusanyika kutoa rambirambi. Waumini wamesimama pamoja kutoa heshima za mwisho huku viongozo wa Kanisa, pamoja na Mapadre, wakiwongoza katika ibada za sala na nyimbo za maombolezo.
Mwadhama Polycarp Pengo alihusiana moja kwa moja na maendeleo ya kiroho, elimu na huduma za kijamii katika taifa, na kifo chake kimeachia pengo kubwa katika Kanisa Katoliki Tanzania. Tarehe ya mazishi inatarajiwa kuwa fursa ya kuenzi maisha na utumishi wake wa kipekee.
Endelea kutembelea tovuti yetu kwa picha zaidi za tukio, taarifa za moja kwa moja kutoka Kanisa na ripoti za kihistoria kuhusu maisha na utumishi wa Kardinali Pengo.
