TAKUKURU Temeke llivyochukulia Hatua Kero ya Wananchi Buza

Bukos Richard
February 27, 2026
0 Comments

Dar es Salaam: 27 Machi 2026, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa TAKUKURU wa Temeke jana umetoa taarifa kufuatia kero ya Wananchi wa Buza inayosambaa mitandaoni.
Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari jana Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa TAKUKURU Temeke, Holle Makungu amesema kero ya wananchi hao ni kukatishwa kwa njia za magari ya abiria maarufu kama daladala katika njia ya Buza -Tandika pamoja na njia za Buza Kanisani.
Makungu amesema hatua hiyo imeelezwa kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi wa eneo hilo wakiwemo wanafunzi wa Shule za Sekondari Keko wanaotoka maeneo ya Mwanagati na Kipera amesema Makungu.
Ameendelea kusema kutokana na malalamiko hayo tayari TAKUKURU imeshatuma timu ya maafisa wake kufanya ufuatiliaji wa kina ili kubaini ukweli wa suala hilo na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.
TAKUKURU imewaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maafisa hao wanaofanya uchunguzi huo ili kuwezesha upatikanaji wa suluhisho la kudumu.
Aidha alisema kwa mamlaka waliyopewa chini ya kifungu cha 7 (a) cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa cha Mwaka 2007 wanazishauri mamlaka zinazohusika na utoaji wa leseni za njia hizo zinazolalamikiwa kuruhusu utaratibu wa zamani kuendelea mpaka uchunguzi utakapokamilika.
Baada ya hapo watatoa ushauri rasmi kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.
Makungu alimalizia kwa kusema TAKUKURU itaendelea kusimamia uwajibikaji na kulinda maslahi ya wananchi kwa kuhakikisha haki na taratibu zinafuatwa.